2 Timothy 3:10-15

10 aLakini wewe umeyajua mafundisho yangu, mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu, upendo, ustahimilivu, 11 bmateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12 cNaam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Al-Masihi Isa atateswa. 13 dLakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14 eBali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani, 15 fna jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Al-Masihi Isa.
Copyright information for SwhKC